Home Simba SC MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO WATIA TIMU DAR NA TAJI LAO

MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO WATIA TIMU DAR NA TAJI LAO

 MABINGWA wa Kombe la Shirikisho,  Simba tayari wameshawasili Dar na taji hilo baada ya kulitwaa jana.

Katika mchezo wa Kombe la Shirikisho kwenye fainali walikutana na Yanga ambao ni watani zao wa jadi.

Ushindi wa bao 1-0, Uwanja wa Lake Tanganyika kupitia kwa Taddeo Lwanga ulitosha kuwafanya watetee taji hilo.

Ikumbukwe kwamba walitwaa msimu wa 2019/20 zama za Sven  Vandenbroec,  Sumbawanga kwa ushindi mbele ya Namungo na jana ilikuwa mbele ya Yanga.

Kocha wa sasa ambaye ni Didier Gomes amesema kuwa ni furaha kwake kuona wanatimiza lengo ambalo walijiwekea.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO MORRISON ALIVYOZIGEUZA SIMBA NA YANGA KUWA KITEGA UCHUMI CHAKE..AKOMBA NUSU BILIONI KILAIINI...