Home Yanga SC YANGA YATAJA POINTI INAZOZITAKA BONGO NDANI YA LIGI

YANGA YATAJA POINTI INAZOZITAKA BONGO NDANI YA LIGI


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utasepa na pointi sita zote ambazo wanazipambania kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara ili kutimiza malengo yao ambayo wamejiwekea.


Ikiwa inanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi imekusanya pointi 70 baada ya kucheza mechi 32, imebakiza mechi mbili zenye pointi sita ni mbele ya Ihefu FC na Dodoma Jiji.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa namna ambavyo wamejipanga wana uhakika wa kusepa na pointi zote sita ambazo wanazipambania.

“Nikuhakikishie kwamba mechi zetu mbili ambazo zimebaki hapo tuna uhakika wa kuchukua pointi zote sita hii yote inatokana na maandalizi mazuri ambayo tumefanya.

“Kikubwa ni kuona kwamba kwenye kila mechi tunafanya vizuri na hilo lipo wazi ukizingatia kwamba kila mchezaji anatimiza majukumu yake anayopewa,” amesema Bumbuli.


Ikiwa Yanga itasepa na pointi zote sita itafanya ifikishe jumla ya pointi 76 kwa kuwa sasa ina pointi 70 baada ya kucheza mechi 32.

Bingwa ni Simba mwenye pointi 79 ametangazwa jana akiwa na mechi mbili mkononi kwa sababu pointi ambazo amezifikia kwa sasa haziwezi kufikiwa na timu yoyote ndani ya Bongo.

SOMA NA HII  YANGA YASHUSHA PRESHA MASHABIKI WAKE, KUREJEA KWENYE UBORA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here