Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…TANZANIA PRISOSN WAKUMBUSHA YA KAGERA NA MBEYA CITY….

KUELEKEA MECHI DHIDI YA SIMBA…TANZANIA PRISOSN WAKUMBUSHA YA KAGERA NA MBEYA CITY….


KOCHA Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba, amebainisha kuwa kwa sasa wamewekeza nguvu na umakini kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Simba ili kuhakikisha wanapata ushindi na kujitoa kwenye nafasi ya mwisho ya msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Februari 3, mwaka huu ambapo Prisons watakua wageni wa Simba kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti la  Spoti Xtra, Kazumba alisema: “Baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rhino Rangers, wachezaji wamefanikiwa kurudisha morali yao kwa sababu tulikuwa na mwenendo usioridhisha kwenye michezo iliyopita ya ligi.

“Simba ni timu nzuri, tunawaheshimu lakini na sisi pia tuna kikosi bora, tutahakikisha tunawapa ushidani, matokeo yatajiweka wazi ndani ya dakika 90.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA ASEC ....MASTAA HAWA SIMBA WAPEWA 'HIRIZI' ZA MCHEZO MAPEMAAA....