Home Azam FC ALIYEKUWA STAA WA RAJA CASABLANCA AFUNGUKA ISHU YAKE YA KUJA BONGO…TIMU YAKE...

ALIYEKUWA STAA WA RAJA CASABLANCA AFUNGUKA ISHU YAKE YA KUJA BONGO…TIMU YAKE MPYA HII HAPA..

Tetesi za Usajili Bongo

Kiungo kutoka nchini Gambia Gibril Sillah, amechimba mkwara mzito baada ya kuweka mazingira mazuri ya kutua Azam FC msimu ujao 2023/24, kwa kusema anakuja kuuwasha moto Bongo.

Uongozi wa Azam Juni 28, mwaka huu ulitangaza kufikia makubalino na Sillah ambaye anatarajiwa kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu zote za usajili na kuanza kuitumikia timu hiyo.

Sillah ambaye atajiunga na Azam FC akitokea klabu ya Raja Casablanca, msimu uliopita akicheza kwa mkopo kwenye kikosi cha JS Soualem kinachoshiriki Ligi Kuu ya Morocco, alihusika kwenye mabao 11 akifunga mabao saba na kutoa pasi za mabao nne.

Sillah amesema: β€œNatarajia kuja Tanzania hivi karibuni kwa ajili ya kukamilisha taratibu mbalimbali za usajili wangu, nafahamu Azam ni miongoni mwa timu zenye malengo makubwa msimu ujao.

β€œHivyo niwatoe hofu mashabiki wa Azam kwa kuwaahidi kupambana na kushirikiana na wenzangu kuhakikisha tunafanya vizuri na kufikia malengo yetu, binafsi niko tayari kuanza kazi rasmi Tanzania.”

SOMA NA HII  JEZI MPYA ZA SIMBA ZATUA RASMI BONGO....