Home Habari za michezo SIMBA QUEENS vs YANGA PRINCESS KITAUMANA TENA KESHO….JE JWANGANI WATAIONEA TENA MSIMBAZI?

SIMBA QUEENS vs YANGA PRINCESS KITAUMANA TENA KESHO….JE JWANGANI WATAIONEA TENA MSIMBAZI?

Simba Queens vs Yanga Prinses

DAKIKA 90, kesho zitaamua nani mbabe katika Derby ya Kariakoo kati ya Simba Queens dhidi ya Yanga Princess mchezo wa mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Simba Queens ni wenyeji wa mchezo huo, itawakaribisha Yanga Princess katika dimba la Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam saa 10:00 Alasiri.

Kwa msimu huu timu hizo zinakutana mara ya pili, walikutana katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii ambapo Simba Queens alifanikiwa kwenda fainali kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bao 1-1.

Simba Queens ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii akimfunga Bingwa mtetezi JKT Queens na Yanga Princes akiibuka mshindi wa tatu akimfunga Fountain Gate Princess.

Simba Queens na Yanga Princess tayari zimecheza mechi mbili za kila kila mmoja na wote wamefanikiwa kukusanya alama sita katika michezo hiyo ya ligi kuu ya Wanawake.

Kila timu ipo imara katika safu yake ya ushambuliaji, Simba Queens katika michezo miwili ya Ligi hiyo jumla amefunga mabao 10 na kuruhusu mabao 2 wakati Yanga Princess walitikisha nyavu mara nane na kuruhusu bao moja.

Kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amesema ni mechi ngunu na ushindani mkubwa kwa sababu ya timu zote mbili zinahitaji pointi tatu kila mmoja kufikia malengo.

Amesema wachezaji wake wako tayari kwa ajili ya kupambania timu ili kutafuta ushindi dhidi ya Yanga Princess ambayo iko imara katika kila nafasi.

“Tunahitaji kurejesha heshima yetu, ili kufikja malengo hayo lazima tupambane tushinde, tunawaheshimu Yanga Princess ambao wako vizuri lakini kikubwa tunahitaji pointi tatu muhimu.

Tutafanya mabaduliko makubwa ya kukosi ambacho kilicheza mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii, tunaingia kivingine na tumejipanga vizuri kwa msimu huu kufikia malengo yetu,” amesema Mgosi.

Aliongeza kuwa mipango na mikakati yetu itabaku kuwa siri ya benchi la ufundi lakini kazi kubwa imefanyika kuandaa kikosi na kutarajia kufanya ushindi.

“Kikubwa tunatafuta alama tatu iwe idadi ya mabao yeyote yale, wakiingia kwenye mfumo basi tutaweza kufunga idadi ya mabao mengi zaidi, mechi itakuwa nzuri na ufundi ndani ya uwanja,” amesema Kocha huyo.

Nahodha wa Simba Queens, Violeth Nicholas amesema wamejiandaa vizuri na wako tayari kupambana kusaka alama tatu muhimu dhidi ya Yamga Princess.

Kocha Mkuu wa Yanga Princess. Charles Haalubono amesema wamejiandaa na anaimani utakuwa mchezo mzuri na wa ahitaji matokeo mazuri mbele ya Simba Queens.

Amesema kila mechi lazima iwe na presha hata unapocheza na timu ndogo wanaweza kukupa mechi mgumu kikubwa ni jinsi ya maandalizi ambayo wamejiandaa.

“Hatuna majeraha na mashabiki wajitokeze kusapoti itakuwa mechi nzuri na ushindani kwa sababu ya kila mmoja kuhitaji matokeo mazuri ya alama tatu muhimu,” amesema Haalubono.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPANGWA NA TIMU YA KINA CHAMA CAF...SIMBA WAJA NA MKAKATI HUU WA KIMFYA...WAIOTA ROBO KWANZA...