Home Uncategorized MBELGIJI WA YANGA AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA LIPULI

MBELGIJI WA YANGA AZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA LIPULI


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kupata ushindi mbele ya Lipuli ya Iringa.

Yanga itacheza na Lipuli majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wao wa kwanza msimu kukutana mzunguko wa kwanza.

“Hakuna kitu kizuri ambacho tunafikiria zaidi ya kupata matokeo mazuri,tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo nasi pia tunapenda kuona timu inashinda,” amesema. 

 Mchezo wa mwisho walishinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa na bao la ushindi lilifungwa na David Molinga aliyemalizia pasi ya Ditram Nchimbi dakika ya 50.

SOMA NA HII  MABINGWA SIMBA KUKWEA PIPA IJUMAA KUWAFUATA UD SONGO KWA 'DEGE' LA KUKODI