Home Uncategorized MBEYA CITY YAZITAKA POINTI TATU ZA KMC

MBEYA CITY YAZITAKA POINTI TATU ZA KMC

MBEYA City leo watakuwa na kibarua cha kutafuta pointi tatu mbele ya KMC ambayo nayo inazitafuta pointi tatu kwa udi na uvumba.

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Amri Said amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na wanaamini watapata matokeo mbele ya wapinzani wao.

“Tunatambua kwamba mchezo wetu wa leo ni mgumu ila tunahitaji kupata matokeo chanya yatakayotufanya tujinasue kwenye nafasi ambayo tupo kwa sasa.

“Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo tunawaomba mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Mchezo wao uliopita Mbeya City ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC.

SOMA NA HII  JEMBE LA KAZI LINALOKUJA YANGA HILI HAPA