Home Uncategorized NAMUNGO FC MAJALIWA WABISHI KINOMANOMA

NAMUNGO FC MAJALIWA WABISHI KINOMANOMA


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa ni kwenye Uwanja wao wa Majaliwa hakuna kilichofukiwa zaidi ya jitihada za wachezaji kutafuta matokeo.
Kwenye mechi tisa ilizocheza Uwanja wa Majaliwa msimu huu, imeshinda mechi saba na kutoa sare moja na  imefungwa mechi moja na mbishi wake akiwa ni Coastal Union kutoka Tanga.
 Thiery amesema kuwa hakuna walichofukia kwenye uwanja wao wa nyumbani zaidi ya wachezaji wake kujituma na kutumia vema Uwanja wa nyumbani.
“Ligi ni ngumu na tunatambua kwamba tukiwa ugenini tunapata tabu kupata matokeo kwa kuwa wenyeji wanakuwa na mashabiki wao ila sisi hatuna hivyo tukiwa nyumbani tunapambana kupata ushindi,” amesema.
Mechi ilizocheza Uwanja wa Majaliwa imefunga jumla ya mabao 13 na kufungwa mabao matano, leo ina kazi mbele ya Alliance FC mchezo utakaochezwa uwanjani hapo.
Matokeo ya Uwanja wa Majaliwa yapo namna hii:- Namungo 2-1 Ndanda, Namungo 2-0 Singida United, Namungo 0-0 Mwadui,  Namungo 1-0 Lipuli, Namungo 1-0 Mtibwa Sugar, Namungo 2-1 Ruvu Shooting, Namungo 1-3 Coastal Union, Namungo 1-0 Polisi Tanzania, Namungo 3-0 Mbao.
SOMA NA HII  SIMON MSUVA ATAMBA KUWA STAA KWENYE CHANGAMOTO MPYA