Home Simba SC KUELEKEA MECHI DHIDI YA WAIVORY…SIMBA YAWAPIGIA MAGOTI YANGA…AHMED ALLY AFUNGUKA A-Z…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA WAIVORY…SIMBA YAWAPIGIA MAGOTI YANGA…AHMED ALLY AFUNGUKA A-Z…


UONGOZI wa Simba umewakaribisha mashabiki wa timu mbalimbali ikiwemo Yanga kuwaunga mkono katika mchezo wao wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast, unaotarajiwa kufanyika Februari 13, katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba inatarajiwa kucheza mchezo huo ambao ni wa kwanza wa Kundi D ambapo timu nyingine ambazo zipo katika kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco na Union Sportive Gerndamarie ya nchini Niger.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba,AhmedAlly, alisema: “Nawakaribisha mashabiki wa timu zote kuja kutushangilia, sio tu mashabiki wa Simba japo naamini kuwa Simba tuna mashabiki wengi sana ambao wangetosha kuja lakini hata wale wengine pia mnakaribishwa kuja kutushangilia.

“Kwetu michuano ya kimataifa si jambo geni na tumezoea kushiriki, safari hii tunahitaji kuona tunafika mbali katika michuano hii, hivyo tumejipanga kupambana katika mchezo huo kuhakikisha kuwa tunafikia malengo yetu katika michuano hii mikubwa baraniAfrika.”

SOMA NA HII  MIGNE ATAJWA KUWA MRITHI WA MIKOBA YA KAZE YANGA