Home Habari za michezo KISA MAFANIKO YA YANGA CAF…TIMU ZOTE LIGI KUU ZASIMAMISHWA KUCHEZA MECHI ZAO…

KISA MAFANIKO YA YANGA CAF…TIMU ZOTE LIGI KUU ZASIMAMISHWA KUCHEZA MECHI ZAO…

Habari za Yanga SC

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuwa mechi za mwisho za msimu wa 2022/23 wa Ligi Kuu ya NBC zitachezwa Juni 9 badala ya Mei 28 ili kutoa nafasi kwa Yanga kucheza michezo yake ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mamlaka hiyo imesema imelazimika kuchukua uamuzi huo ili kuhakikisha uwepo wa haki na usawa michezoni na kuondoa mazingira yanayoweza kuashiria upangaji wa matokeo katika michezo hiyo ya Mwisho.

Aidha, mabadiliko hayo yanakwenda sambamba na mabadiliko ya michezo ya mzunguko wa 29 ambapo sasa timu zote zitacheza Juni 6 mwaka huu.

Yanga itashuka dimbani Mei 28 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo wake wa kwanza wa fainali dhidi ya USM Alger ya Algeria, ambapo zitarudia tena Juni 3 nchini Algeria.

SOMA NA HII  KISA SARE TATU MFULULIZO....MWAMNYETO NAYE KASHINDWA KUJIZUIA YANGA...KAAMUA KUANIKA HAYA MAPYA...