Home Habari za michezo AHMED ALLY AMTABIRIA BALEKE MVUA YA MAGOLI

AHMED ALLY AMTABIRIA BALEKE MVUA YA MAGOLI

Habari za Simba leo

Akiwa tayari ashapachika wavuni mabao 2 katika michezo miwili ya Ligi aliyocheza Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke.

Tayari wanasimba wameshamuwekea matumaini makubwa wakijinasibu kuwa moto alioanza nao hauwezi kuzikmika kirahisi.

Miongozi mwao ni Ofisa Habari wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally ambae amesema kuwa msimu huu Straika huyo atafunga mabao 30.

Akizungumza Ahmed anasema;

“ Ninamtabiria makubwa mshambuliaji wetu Baleke msimu huu,ninaamini atafunga mabao kuanzia 30, hiyo ni kutokana na mwanzo mzuri alioanza nao, ”

“ Sio kitu kidogo kwake kufunga mabao mawili ndani ya michezo miwili, akiendelea kufanyia kazi maelekezo na mafunzo mazoezini, basi atafunga katika kila mchezo wa ligi, Kikubwa anachotakiwa kukifanya kuendelea na hapo alipoanzia, asibweteke na idadi ya mabao atakayoyafunga, ”

Je, unadhani Baleke atafunga mabao mangapi msimu huu?

SOMA NA HII  UCHOCHORO WA SIMBA KUWA KIBONDE UKO HAPA