Home Simba SC SIMBA QUEENS WAINYOOSHA YANGA PRINCES GOLI 3-0

SIMBA QUEENS WAINYOOSHA YANGA PRINCES GOLI 3-0


Mabingwa  watetezi wa Ligi Kuu ya wanawake Tanzania , Simba Queens wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya watao zao wa jadi Yanga Princess katika mchezo wa mzunguko wa 15 uliochezwa leo katika uwanja wa Uhuru.

Simba Queens ambao wako chini ya Kocha Mkuu, Mussa Hassan ‘Mgosi’ walianza kuyahesabu magoli yao,katika dakika ya 29 kupitia kwa nahodha wake, Mwanahamis Omary.

Katika dakika ya 42, Mchezaji Oppa Clement aliifungia Simba Queens goli la pili kwa njia ya penalti mara baada ya nahodha wa Yanga Princes Happyness Mwaipaja ‘kuunawa’ mpira akiwa katika harakati za kuzuia shuti la Mwanahamis Omary.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Simba Queens kuwa mbele kwa goli 2-0, Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote mbili kushambuliana kwa kasi, ambapo iliwachukua dakika 10 Simba Queens kuandika goli la tatu kupitia kwa kiungo wake fundi, Joele Bukuru.

Aidha,katika mchezo huo ulikokuwa mkali kwa pande zote mbili,mashabiki wa pande zote mbili wamejitokeza kwa wingi katika kuzipa hamasa timu zao, huku wale wa Simba Queens wakionekana kuwa wengi zaidi ya Yanga Princess.

Kwa ushindi huo,Simba Queens imepanda mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na jumla ya alama 39, huku ikifuatiwa na Yanga Princes yenye alama 38.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA SIO ONYANGO TU....SADIO KANUOTE NAYE HAJAENDA NA TIMU SUDANI....YEYE KAAMUA KWENDA KWAO KABISA...