Home Habari za michezo MASHINE MPYA YA MAGOLI SIMBA HII HAPA….KULIPWA MSHAHARA WA MIL 210 KWA...

MASHINE MPYA YA MAGOLI SIMBA HII HAPA….KULIPWA MSHAHARA WA MIL 210 KWA MWAKA…

Habari za Usajili Simba

UONGOZI wa Simba umemtambulisha mshambuliaji mpya Pa Omar Jobe akitokea katika klabu ya FC Zhence inayoshiriki Ligi Kuu, Kazakhstan.

Jobe ni raia wa Gambia nchini humo akijulikana kwa jina la utani Drogba moja ya rekodi yake kuwa mfungaji bora wa ligi ya Senegal alipokuwa akicheza pamoja Babacar Sarr kwenye ligi hiyo kabla ya kwenda Ulaya.

Inaarifiwa kuwa Jobe amesaini mkataba wa Miaka miwili wenye kipengele cha kuongezeka endapo atakuwa na kiwango kizuri.

Aidha pia, Jobe atakuwa akilipwa mshahara wa dola 7000 kwa mwezi ambazo ni sawa na Tsh Milioni 17.5 ambapo ukizidisha mara miezi 12 atakuwa akilipwa Mil 210, huku akipewa pia nyumba ya kishua, gari ya kutembelea na bonasi ya Tsh laki 200,000 kwa kila mechiĀ  ambazo Simba watashinda kwa ligi ya NBC na kombe la ASFC.

Pia kulingana na bonasi kwenye klabu ya Simba, Jobe atakuwa akilipwa posho ya Tsh laki 4 mpaka 5 kwa kila mechi moja ya kimataifa ambayo timu itakuwa inashinda huku yeye akiwa ni sehemu ya mchezo.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema idara ya ushambuliaji ni moja ya eneo ambalo kocha Abdelhak Benchikha alitaka walifanyie maboresho na wamefanikiwa kumleta Jobe.

Amesema usajili uliofanywa ni mapendekezo ya benchi la ufundi, ujio wa Jobe mchezaji wa pili wa kimataifa kusajiliwa dirisha dogo baada ya Babacar amesajili kutoka US Monistir.

“Jumla tumesajili wachezaji wanne na wazawa wawili akiwemo Salehe Karabaka na Ladack Chasambi, tumeimarisha kila sehemu kama mapendekezo ya kocha.

Wapo wachezaji ambao tutachana nao kwa sababu mashindano ya kombe la Mapinduzi imempa kocha mwanga wa kuona mchezaji gani anaondoka na nani anabaki ndani ya kikosi,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa wamepoteza kombe la Mapinduzi ila wamepata faida kubwa kwa sababu kuna wametega milango yao ijayo katika ligi kuu, kombe la FA na kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  CHAMA: SIMBA WANAWEZA KUZIBA PENGO LANGU....