Home Yanga SC MUKOKO : NILICHEZA DHIDI YA COASTAL UNION NIKIWA MAUMIVU MAKALI

MUKOKO : NILICHEZA DHIDI YA COASTAL UNION NIKIWA MAUMIVU MAKALI


Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe amesema kama kuna mchezo umemuumiza basi ni dhidi ya Coastal Union ambao amecheza huku akiwa na maumivu.

Mukoko amesema katika mchezo huo wa jana ambao Yanga ililala kwa mabao 2-1 ikiwa na kipigo chao cha kwanza kwenye ligi alikuwa na maumivu makali ya jino.

“Kulikuwa na upepo mkali ambao ulikuwa unaongeza maumivu zaidi nikasema hakuna namna lazima niipiganie timu” amesema kiungo huyo na kuongeza

“Niliona ugumu wa mchezo nikaona kama nitatoka nitawaumiza mashabiki na hata wachezaji wenzangu nikajikaza na kupambana,”

Kiungo huyo Mkongomani amesema matokeo ya kupoteza mchezo huo yamemuumiza zaidi  ukichanganya na maumivu aliyonayo.

Aidha Mukoko amesema hakuna namna zaidi ya kurudisha ubora wao uwanjani ambapo amewaomba radhi mashabiki wao kwa hatua hiyo ya kupoteza mchezo huo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMTAMBULISHA MBURUNDI WA NEWCASTEL JANA...MASHINE NYINGINE HII HAPA ITATUA YANGA...BANDO MUHIMU...