Home Yanga SC SARPONG AONGEZA LISTI YA MAJERUHI YANGA

SARPONG AONGEZA LISTI YA MAJERUHI YANGA


Wakati Yanga ikitua jijini Arusha tayari kwa mchezo dhidi ya wenyeji wao Polisi Tanzania idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka wakati wowote ndani ya timu hiyo kufuatia kuumia kwa mshambuliaji Michael Sarpong.

Sarpong aliumia katika mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union baada ya kugongana na beki Hans Masoud akitolewa dakika ya 32 nafasi yake ikichukuliwa na Yacouba Sogne,mchezo ambao Yanga ilikubali kipigo cha kwanza msimu katika ligi kuu kwa mabao 2-1.

Wakati Yanga ikiondoka Mkoani Tanga Sarpong alionekana akichechemea mguu mithili ya mtu ambaye bado ana maumivu makali katika mguu wake wa kulia.

Wakati mshambuliaji huyo akielekea kwenye basi makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Yanga Hersi Said amesema kwa mujibu wa madaktari wao bado hawajajua kama mshambuliaji huyo ataweza kuwa sawa kabla ya mchezo ujao.

Hersi amesema amefuatilia afya ya mchezaji huyo na kujulishwa kwamba atalazimika kusubiri taarifa ya mwisho ambayo inaweza kutoka kesho.

“Hakuna uhakika amepata maumivu makali lakini madaktari wanahangaika kumpa uponaji tutajua kesho tukiwa Arusha,” amesema Hersi.

Hatua ya Sarpong kuwa majeruhi anaungana na Said Ntibazonkiza,Ditram Nchimbi sambamba na Mapinduzi Balama ambaye bado anauguza majeraha ya muda mrefu

SOMA NA HII  KWA MATUKIO HAYA TU....AUCHO APEWE UNAHODHA WA YANGA HARAKA SANA....