Home news KUELEKEA MECHI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA…SIMBA WAPEWA KIBALI MAALUMU NA CAF..UONGOZI...

KUELEKEA MECHI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA…SIMBA WAPEWA KIBALI MAALUMU NA CAF..UONGOZI WAANIKA HAYA..


SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 35, 000 kuhudhuria mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast utakaopigwa Februari 13 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

CAF imeitaka klabu hiyo kufuata taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa corona kama kukaa kwa nafasi baina ya mtu na mtu, kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji safi na vitakasa.

Aidha CAF imesisitiza taratibu hizo kuzingatiwa hivyo kila shabiki anapaswa kuchukua hatua na kumlinda mwenzake aliye karibu yake kwa muda wote wa mchezo huo.

Katika hatua nyingine uongozi wa klabu hiyo umepanga kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika huku ukiwataka mashabiki kununua tiketi mapema ili kuondoa usumbufu siku ya mchezo.

Simba imepangwa kwenye kundi D katika michuano hiyo ikiwa na timu za RS Berkane (Morocco), Asec Mimosas (Ivory Coast) na US Gendarmerie Nationale ya Nigeria.

Baada ya mchezo na Ases Mimosas, Simba itasafiri kucheza michezo miwili ugenini na US Gendarmerie Nationale Februari 20 kisha RS Berkane Februari 27, kabla ya kurudiana na Berkane Machi 13 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Michezo miwili iliyosalia itasafiri Ivory Coast kucheza na Ases Mimosas Machi 20, kisha kumaliza hatua hiyo ya makundi dhidi ya US Gendarmerie Nationale Aprili 3 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  MKWANJA WA KUTOSHA WAWEKWA MEZANI NA GSM KISA WANAIJERIA