Home Simba SC MO DEWJI ATIBUA DILI LA GOMES KWENDA RAJA CASABLANCA YA MOROCCO

MO DEWJI ATIBUA DILI LA GOMES KWENDA RAJA CASABLANCA YA MOROCCO


BILIONEA wa Simba, Mohammed ‘Mo’ Dewji juzi aliwapa furaha kubwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo, baada ya kukabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni iliyokuwa ikiwatoa watu pozi, lakini kumbe siku chache alifanya kazi ya ziada kumzuia Kocha Mkuu wa Didier Gomes asalie kikosini.

Inaelezwa, kabla ya kumtika kwenye mapumziko nchini kwao Ufaransa, Gomes alifanya kikao kizito na Mo Dewji na kumjulisha juu ya kuwepo kwa ofa nne za kutakiwa na klabu kadhaa maarufu Afrika ikiwamo wababe wa Morocco, Raja Casablanca.

Gazeti la Mwanaspoti limepenyezewa taarifa za uhakika kutoka Simba ambazo zilifanywa siri kubwa, kuwa Gomes alipata ofa hizo baada ya klabu hizo kuwasiliana na wakala wake na kutangaza dau lao la mkwanja mrefu na Mfaransa huyo akaona awasilishe kwa bilionea huyo wa Simba.

Inaelezwa Raja walikuwa tayari kununua mpaka mkataba wa wa Gomes ambao bado haujamalizika Msimbazi ilimradi wafanye naye kazi.

Mbali na Wamorocco klabu nyingine zinazomfukuzia Gomes aliyeajiriwa Simba Januari mwaka huu akitokea El Merreikh ya Sudan ni Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns za Afrika Kusini pamoja na timu ya taifa ya Sudan.

Ndipo Mo Dewji aliamua kumpa mkataba mwingine mpya utakaomfanya awepo klabu hapo hadi msimu wa 2022-2023.

“Gomes baada ya kufanya kikao na Mo Dewji walikubaliana kusaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kuendelea kusalia hapa Simba na kuachana na mipango ya kwenda katika timu nyingine,” kilisema chanzo chetu na kuongeza;

“Gomes aliondoka nchini Julai 26, kwenda kwao Ufaransa lakini kabla ya kuanza safari hiyo masaa machache yaliyopita ndio alisaini mkataba huo wa mwaka mmoja na mwenyewe ameeleza kuwa na mapenzi makubwa Simba licha ya ofa nano alizokuwa nazo kuzipiga chini.”

Chanzo hicho cha kuaminika kilidokeza pia; “Baada ya kuongeza mwaka mmoja nasi ameonekana kufurahi na ameondoka kwao Ufaransa atarejea nchini siku chache kabla ya Agosti 10, siku ambayo tutaanza safari ya kwenda Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA YANGA WAKITAMBA SANA...SAKHO KWA HASIRA KANG'ATA MENO..KISHA AKASEMA HAYA...

Awali, Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez aliliambia Mwanaspoti uongozi umepanga kuwekeza nguvu katika maeneo yote ya msingi ikiwemo benchi la ufundi, ili kuhakikishan msimu ujao wanafanya mambo makubwa zaidi ya yale iliyofanywa kwa misimu minne mfululizo iliyopita.

“Tumepanga kulipatia kila benchi letu la ufundi wanachohitaji ili kuona tunafanya vizuri katika kila mashindano ambayo tunashiriki kwani hayo ndio malengo ya klabu.”