Simba SC

CHAMA AKUTANA NA JOTO YA JIWE, KISA HAJI MANARA, MO APIGA MKWARA

admin August 7, 2021 10:43 am


 STAA wa Simba, Clatous Chama, Agosti 6, 2021 ameonja joto la jiwe baada ya kuchenjiwa kibao na muwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kisa Haji Manara.

 

Chama akiwa Live Insta kwenye mkutano wake na mashabiki ambao Mo alikuwemo, aliulizwa swali kuhusu kuondoka kwa Haji Manara ndani ya Klabu ya Simba, kwenye kujibu Chama alimsifia Haji kitendo ambacho kilionekana kumchefua sana Mo.



Mo alimuuliza Chama “Haji ndiye aliyekulipia ada ya uhamisho?” Chama akiwa anamjibu Mo, alijibu kwa kuomba msamaha kama amemkwaza, Mo akamuuliza tena Nani aliyekulipia Ada….Haji? baadaye Chama alipotaka kujibu Mo akamwambia anatoka kwenye mkutano huo.


Ndani ya ligi nyota huyo amehusika kwenye mabao 23 akifunga mabao 8 na kutoa pasi 15 za mabao kati ya mabao 78.

Kwa sasa inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za Kaizer Chiefs pamoja na timu ya kutoka Morocco inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ya FAR Rabat.

VIDEO:MOHAMED HUSSEIN AUGA UKAPERA, AFUNGA NDOA KISA LUIS  MIQUISSONE …CHAMA ATANGAZA KUSEPA MSIMBAZI, BARBARA ATOA NENO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply