news

ALIYEKATWA KUGOMBEA URAIS APEWA UJUMBE

admin August 8, 2021 11:43 am


 HAWA Mniga ambaye alichukua fomu kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ameteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya utendaji.

 

Baada ya kuidhinishwa jana Agosti 7 kuwa rais wa TFF kwa awamu ya pili, Wallace Karia amewateua wajumbe wanne kuingia kwenye kamati Tendaji akiwamo Hawa, ambaye alijitosa kuwania urais kwenye uchaguzi huo na jina lake kukatwa kwenye usaili kwa kukosa sifa ya uzoefu.


Hawa awali alibainisha kwamba anahitaji kufanya kazi kubwa ya kuongoza mpira wa Tanzania kwa kuwa ana uzoefu katika masuala ya uongozi. 


Kwa sasa anakuwa ni miongoni mwa wajumbe wanne walioteuliwa na Rais baada ya zoezi la kumuidhinisha Karia kuendelea kuongoza Shirikisho hilo kufanyika mjini Tanga.


Wengine aliowateua ni Athuman Nyamlani ambaye alimteua pia kuwa Makamu wa Rais wa TFF kwa miaka minne ijayo.


Wajumbe wengine walioteuliwa na Rais ni Ahmed Mgoyi na Said Sudi.


SIMBA YAMPELEKA GYM SMSHAMBULIAJI WAKE MPYA MESSI AMWAGA MACHOZI AKIWAAGA MASHABIKI BARCELONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply