kimataifa

MESSI AMWAGA MACHOZI AKIWAAGA MASHABIKI BARCELONA

admin August 8, 2021 12:43 pm


 WIMBO wa mkongwe wa muziki wa Country, Don Williams wa Fare Well Jamaica ndiyo uliomkaa mshambuliaji wa Dunia, Lionel Messi ambaye amejikuta akiangua kilio mbele ya vyombo vya habari wakati akiwaaga mashabiki na viongozi wa Barcelona.


Leo mchana, Messi aliandaliwa mkutano kwenye viunga vya Camp Nou kwenye maskani ya timu hiyo ambapo ameshindwa kabisa kuzuia hisia zake na kujikuta anashindwa aseme maneno gani ya kwaheri Kwa Wana-Barcelona na badala yake akajikuta akiangua kilio kama mtoto mdogo.

 

Ni ngumu kuamini ila ndiyo hivyo, Barcelona na Messi ambaye ameitumikia klabu hiyo tangu utotoni hadi amekuwa mbaba, wanaachana katika nyakati ngumu sana.


Nyota huyo ambaye amecheza ndani ya Barcelona kwa zaidi ya miaka 20 alikuwa tayari kuongeza dili jipya la miaka mitano lakini kutokana na kuyumba kwa uchumi wa Barcelona uliosababishwa na janga la Corona ulifanya shughuli iwe nzito.


La Liga walipoutazama mkataba mpya wa Messi waliugomea kwa kuwa ulikuwa na matumizi makubwa ya fedha hasa kwa upande wa mshahara licha ya Messi kukubali kupunguziwa asilimia 50.


Wakati akiwaaga amesema:”Nilitamani kubaki na nilikuwa ninapenda kubaki kwa kuwa kwa muda mrefu tumekuwa familia ila sina chaguo, zaidi ya kusema byebye,” . 

ALIYEKATWA KUGOMBEA URAIS APEWA UJUMBE NABI AANZA NA MAYELE PAMOJA NA MAKAMBO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply