Azam FC

AZAM FC MIKONONI MWA WASOMALIA KOMBE LA SHIRIKISHO

admin August 13, 2021 7:43 pm


KOMBE la Shirikisho (CAF) Klabu ya Azam FC ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika hatua ya awali itakutana na klabu ya Horseed FC kutoka nchini Somalia.

Leo  Agosti 13 Caf imechezesha droo ya mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho nchini Cairo.

 Mshindi wa mtanange huo atakutana na matajiri wa Misri Pyramids FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho. 

Azam FC inayonolewa na George Lwandamina ina kibarua kikubwa katika kupeperusha bendera ya Tanzania katika kuifanya Tanzania kuzidi kupasua anga la kimataifa.

Pia wawakilishi wengine katika Kombe la Shirikisho kutoka Tanzania ni Biashara United ambao watamenyana na DIKHIL.

Mechi za awali zinatarajiwa kupigwa Septemba 10-12.

VIDEO:SIMBA YAMTAMBULISHA NYOTA MPYA YA CHAMA NA MANARA..MO DEWJI ASIOGOPWE AKUMBUSHWE ANAPOKOSEA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply