news

MTIBWA SUGAR HESABU ZAO ZIPO NAMNA HII

admin August 14, 2021 2:44 pm


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba watafanya usajili bora ambao utawafanya wafanye vizuri msimu wa Ligi Kuu Bara wa 2021/22.

Msimu uliopita Mtibwa Sugar ilikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 14 na pointi 39 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.

Ilipata nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa ushindi mbele ya Trasint Camp ambayo inacheza Ligi Daraja la Kwanza ilikuwa ni kwenye mchezo wa play off.

Ilishinda kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 mbele ya wapinzani hao ambao walikuwa wanahitaji kupanda Ligi Kuu Bara.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya maboresho ya kikosi hicho kwa ajili ya mechi zao za ligi.

 

KISA USAJILI MPYA WA YANGA..ZAWADI MAUYA AFUNGUKA HAYA..AMTAJA NIYONZIMA RASMI:SIMBA YATAMBULISHA JEMBE LA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply