Simba SC

SIMBA YAMNASA NYOTA MSENEGAL, KUMPA DILI JIPYA

admin August 14, 2021 8:43 am

 IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,  Didier Gomes imemalizana na nyota kutoka Klabu ya Teungueth ya Senegal Pape Ousmane Sakho.

Nyota huyo ni kijana ambaye ana miaka 24. Taratibu zote za usajili zimefikia pazuri na atajiunga na timu Morocco.

Pape Ousmane Sakho (24)  ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Senegal akiwa na Teungueth walitwaa ubingwa wa ligi. 

Kiungo huyo mshambuliaji anatajwa kuwa mchezaji wa ndani mwenye kipaji kikubwa nchini Senegal.

Ni mabao 8 na pasi 10 alitoa , pia ndiye mchezaji aliyeng’ara wakati timu ya Teungueth ikiitoa timu ya Raja Casablanca ya Morocco msimu ulioisha na kufuzu hatua ya makundi ya Caf Champions League.

Kwa sasa Simba ipo nchini Morocco kwa ajili ya kambi ya msimu wa 2021/22.

KISA CHAMA KUSEPA MSIMBAZI..MANARA ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA KUUZWA KWA  CHAMA NA LUIS KWAWASHTUA WAARABU..HIVI NDIVYO MEDIA ZA HUKO ZINAVYOANDIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply