LIVERPOOL imeanza Ligi Kuu England kwa kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Norwich na kumfanya Kocha Mkuu, Jurgen Klopp kuwapongeza vijana wake kwa matokeo hayo.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Caroww Road ulisoma Norwich 0-3 Liverpool na nyota wa mchezo akiwa ni raia wa Misri, Mohamed Salah ambaye aliweza kuonyesha uwezo mkubwa ndani ya uwanja.
Alitupia bao moja na kutoa pasi mbili ambapo alifunga dakika ya 74 Diogo Jota alitupia dk ya 26 na Roberto Firmino dk 65. Salah anafanikiwa kufunga kwenye jumla ya mechi tano kwenye misimu mitano mfululizo katika mechi za ufunguzi.
Rekodi zionyesha kuwa alianza kufanya hivyo msimu wa 2017/18 mbele ya Watford alitupia bao moja, 2018/19 West Ham United bao moja, 20019/20 Norwich aliwafunga bao moja, 2020/21 Leeds aliwafunga mabao matatu na msimu wa 2021/22 alitupia bao moja.
Inakuwa ni wiki nzuri kwa Liverpool kupata ushindi huo mbele ya Norwich ambao wameshindwa kupata furaha kama ilivyotokea kwa timu Brentford na Watford ambazo zilianza kwa ushindi
Kureja kwa Virgil van Dijk kwa muda katika mechi za mashindano baada ya miezi 10 kunaongeza nguvu kwenye kikosi hicho katika upande wa ulinza,