MZEE wa kuchetua Bernard Morrison amesema kuwa maisha ndani ya Simba ni raha huku akifurahi uwepo wa Jonas Mkude ambaye alikuwa nje ya kikosi kwa muda kutokana na masuala ya nidhamu.
Kwa sasa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kimeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.
Ni mabingwa watetezi wa ligi pia walitwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa ushindi mbele ya watani zao wa jadi Yanga kwa ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa mwisho wa reli Kigoma, Uwanja wa Lahe Tanganyika.
Morrison amesema:”Ninafurahi kuwa ndani ya Simba pia kuwa na kijana kutoka Muhimbili, Jonas Mkude hapa ni furaha kubwa ndani ya Simba.
“Ukimzungumzia Mkude unataja moja ya viungo wakabaji bora Tanzania, hivyo nipo na mchezaji bora kwenye eneo la viungo wakabaji ni furaha tupu,” amesema.
Mkude kutokana na matatizo ya nidhamu ya kujirudiarudia mara kwa mara ndani ya Simba kabla ya kuepa kueleka Morocco ilielezwa kuwa alipaswa kwenda Muhimbili kufanyiwa vipimo.
Kwa sasa yupo nchini Morocco Mkude na alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzo kuripoti kambini, Dar kabla ya timu kuelekea Morocco.