Habari za michezo

KUELEKEA MECHI ZA CAF…SIMBA SC WAANZA UMAFIA MAPEMA….WATUMA JESHI LA ‘VIWAVI’ LILONGWE MALAWI…

admin September 7, 2022 1:46 pm


Simba wako Dar es Salaam kimwili lakini akili na mipango yao yote ipo Lilongwe Malawi.

Katika kuhakikisha wanaanza kwa umakini kabisa kwenye mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets jana Jumanne kuna msafara wa watu maalumu watatangulia Malawi kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.

Msafara huo wa watu maalumu utakwenda kuhakikisha mazingira na vitu muhimu vya ndani ya nje ya uwanja kabla ya timu kufika Alhamisi vinakuwa kwenye mpangilio mzuri na kuepuka fedheha yoyote kutoka kwa wageni ambao wameahirishiwa mechi zao mbili za Ligi ili kujiandaa kikamilifu.

Simba itacheza mechi ya kwanza ya hatua ya awali ugenini Jumamosi ya Septemba 10 kabla ya kurudiana nao Uwanja wa Benjamin Mkapa maarufu kama machinjioni Septemba 17

WAKATI SAKATA LA KISINDA HALIJATULIA…MAKAMBO NA MOLOKO WAWEKWA KWENYE MSITARI WA HATARI YANGA… SAKATA LA KISINDA KUZUILIWA NA TFF…YANGA WASIMAMIA UKUCHA…WALIPA MAMILIONI YA PESA CAF ILI ACHEZE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply