Home news TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU WACHEZAJI 12 WA KIMATAIFA

TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU WACHEZAJI 12 WA KIMATAIFA


WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) amesema kuwa wameongeza idadi ya wachezaji wa kigeni ambao watasajiliwa kwenye timu kwa ajili ya zile ambazo zitashiriki mashindano ya kimataifa.

Ni Simba, Yanga ambazo zitashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam FC na Biashara United wakiwa kwenye Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, jana Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Karia alisema kuwa taarifa za kuongeza wachezaji wa kimataifa zipo na wameongeza kwa malengo maalumu.

“Wameongezwa wachezaji wanakuwa wasiopungua 40 kutokana na Covid situation iliyopo sasa hivi Caf wameamua kuongeza wachezaji kuwa 40.

“Lakini pia baada ya mijadala mingi tumeona kwamba timu zetu ambazo zinashiriki nyingi zimeomba tuongeze wachezaji. Tumeona kwamba tuziruhusu ziende na wachezaji 12 wa kigeni lakini kwenye orodha ya wachezaji 18 watakaocheza mechi za kwetu za ligi watakuwa ni wachezai 8 watakaoorodheshwa kwenye mashindano haya.

“Kwa upande wa mechi za kimataifa wenyewe watakavyotumia lakini kwenye ligi kuu tumepunguza kutoka wachezaji 10 mpaka 8, maana yake wachezaji kwenye ligi ya ndani tumepunguza kwa michezo ya ndani ili kuangalia timu zetu zinaweza kushiriki namna gani zikiwa dhabiti,” alisema Karia.

SOMA NA HII  KIUNGO WA BOLI AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YA YANGA