HERITIER Makambo, nyota mpya wa Yanga amesema kuwa anaamini kwamba atafanya vizuri ndani ya timu hiyo kwa msimu mpya wa 2021/22 katika Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dili lake ni la miaka miwili na aliibuka hapo akitokea Klabu ya Horoya AC ya Guinea ambapo huko alisitisha mkataba wake kutokana na kutokuwa na nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Pia Makambo aliibuka huko Guinea akitokea Tanzania kwa kuwa alikuwa akicheza Yanga zama za Mwinyi Zahera ambaye alikuwa ni Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2018/19.
Wakati anasepa alikuwa ni namba moja kwa utupiaji alitupia mabao 17 ambayo mpaka sasa hakuna mshambuliaji ambaye ameweza kuyafikia kwa kuwa kinara wa msimu huu ni Yacouba Songne mwenye mabao 8.
Yupo kwenye kikosi ambacho kimeibuka nchini Morocco na usiku wa leo kilikuwa Dubai kabla ya kuunganisha safari ya kuelekea Morocco kwa kambi ya maandalizi ya msimu wa 2021/22.
Makambo amesema:”Nina amini kwamba nimerudi ili kuweza kutimiza majukumu yangu ambayo ni kufunga kwa kushirikiana na wachezaji wenzagu.
“Pia ninapenda kuona tunatwaa makombe kwenye mashindano ambayo tutashiriki hivyo kikubwa ni sapoti na tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema.