Home Yanga SC YANGA KAMILI GADO KWA MSIMU UJAO, KAZI INAENDELEA

YANGA KAMILI GADO KWA MSIMU UJAO, KAZI INAENDELEA


 YANGA inaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ikiwa ipo nchini Morocco na imewajumuisha wachezaji wake wapya pamoja na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2020/21.


Miongoni mwa nyota waliopo kambini ni pamoja na Yacouba Songne ambaye ni namba moja kwa utupiaji msimu wa 2020/21 na Zawad Mauya.

Ni mabao 8 alifunga na pasi nne za mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao 12 kati ya 52 ambayo yalifungwa na timu hiyo.

Kwa wale wachezaji wapya ambao wapo kambini ni pamoja na Jesus Muloko ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Tuisila Kisinda ambaye anatajwa kuibukia Morocco. 

Heritier Makambo ambaye aliwahi kucheza Yanga zama za Mwinyi Zahera naye amerejea tena kikosini. 

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

SOMA NA HII  ZA NDANI KABISAA....;'MWAISA' KASEKE KUTUPIWA VIRAGO YANGA...MABOSI WAMCHUNIA ISHU YA MKATABA MPYA...