news

FAMILIA WAWEKA WAZI SABABU YA KIFO CHA MWL KASHASHA..ALILAZWA KWA WIKI MBILI

admin August 20, 2021 5:00 pm


MCHAMBUZI mahiri wa kandanda hapa nchini Mwalimu Alex Kashasha amefariki Dunia jana saa 9 alasili  katika Hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.

Kashasha alikuwa amelazwa Hospitalini hapo wiki mbili zilizopita mpaka umauti ulipomkuta akiwa anapatiwa matibabu.

Akithibitisha kifo hicho Silla Jackson aliyejitambulisha kama rafiki wa familia amesema, taarifa za kufariki kwa Kashasha ni za kweli na sasa wanatarajia kukaa kikao cha familia.

Amesema marehemu amefariki kwa tatizo la figo lililopelekea kulazwa hospitalini hapo na sasa wanapanga taratibu za maziko.

“Mimi ni rafiki wa familia yeye hawezi kuongea na simu lakini kama familia ndio tunajipanga kutoka hapa hospitali kwenda nyumbani ndio tutajua nini kitaendelea,” amesema ndugu huyo.

Kabla ya umauti kumkuta alikuwa akifanya kazi na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pia alikuwa mchambuzi wa gazeti la Mwanaspoti Jumamosi. 

EDO KUMBWEMBE AWACHANA WACHEZAJI WA KIBONGO KISA PESA ZA WAARABU..AMTAJA MSUVA SIMBA YAMPA KAKOLANYA POLE, SISI SOTE NI FAMILIA,POLE KAKOLANYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply