Home Yanga SC KUELEKEA MSIMU MPYA….WACHEZAJI YANGA KUKATWA LAKI MBILI WAKIZINGUA

KUELEKEA MSIMU MPYA….WACHEZAJI YANGA KUKATWA LAKI MBILI WAKIZINGUA


Kocha wa Yanga Nesreddine Nabi amewataka wachezaji wake kuhakikisha kila mmoja anaheshimu muda na katika kusimamia hilo ametangaza adhabu katika maeneo tofauti ambayo atakutana na makosa kwa wachezaji wake.

Kocha Nabi amesema ili Yanga ifikie malengo yake hatua ya kwanza kila mchezaji na watu wake kwenye benchi la ufundi wanatakiwa kuheshimu muda kwa kila eneo kufika kwa wakati bila kuchewlewa.

Raia huyo wa Tunisia amewatangazia wachezaji kama kuna mchezaji atashindwa kuheshimu muda adhabu ya kwanza atakatwa dola 100 (Sh 230,000) kwa kila hatua ya kuchelewa.

“Tunatakiwa kufanya mambo yetu kwa kuheshimu muda hii ndio hatua ya kwanza ya nidhamu yetu,ukiwa na nidhamu ya kuheshimu muda hata uwanjani utakuwa makini na na ndio maana nimewaambia sasa,”amesema Nabi.

“Hii sio kwa wachezaji tu hata sisi watu wa benchi la ufundi nimewaambia kama kuna mtu atafanya makosa atakumbana na dhabu na hili nitasimamia mimi mwenyewe ili mambo yaende kwa haraka.”

SOMA NA HII  JEMBE LA KAZI YANGA LAANZA MATIZI, MANULA ANAJUA SHUGHULI YAKE