Habari za Yanga
Habari za michezo

KUHUSU ISHU YA KUTOLEWA KWA MKOPO….KONKONI AIVIMBIA YANGA…..’SIENDI GHANA’…..

admin January 4, 2024 9:50 am

Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa Konkon anaenda Ghana kwa mkopo ,mshambuliaji huyo amekanusha taarifa hizo kwa kusema.

“Mimi nimeomba tu ruhusa kwa kocha na nikapewa ruhusa ya kuondoka ili niweze kutatua masuala ya familia yangu, nimeomba tu ruhusa nirudi Dar es Salam ili niweze kutatua masuala ya kifamilia nikiwa Dar Es Salaam.”

“Siendi Ghana, nimekuja Dar es Salam ili nitume pesa nyumbani, Kwa sababu nikiwa Zanzibar nimeshindwa kufanya uhamisho wa fedha kwenda nyumbani.”

“Lakini nimeshangazwa na hizi taarifa kama naondoka kwenda Ghana kwa ajili ya usajili wa mkopo jambo ambalo sio kweli, na tayari nipo Dar Es Salam.”

amesema Hafiz Konkoni mshambuliaji wa Yanga SC.

Pamoja na kauli ya Konkoni, lakini inafahamika wazi kuwa Yanga wako kwenye mchakato wa kumalizana naye kwenye dirisha hili dogo ili nafasi yake ichukuliwe na staa mwingine wa kigeni.

Itafahamika kuwa Yanga mpaka sasa imeshatangaza kumsajili Agustine Okrah, ambaye anafanya idadi ya wachezaji wa kigeni Yanga kuwa 13, hivyo lazima mmoja apungue.

Hata hivyo, kuna taarifa za Jesus Moloko kutolewa kwa mkopo kwenda Singida Fauntain Gate , na hii ni kama hakutakuwa na mchezaji mwingine wa kigeni anayesajiliwa, kwani kama kutakuwa na mchezaji mwingine itabidi Konkoni akatwe.

Konkoni toka ajiunge na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, ameshindwa kuwa na kiwango cha kuridhisha ambapo mara kadhaa amekuwa akianzia benchi, au wakati mwingine asicheze.

DUCHU, CHILUNDA NJIA PANDA SIMBA….BENCHIKHA AWAKA HASIRA AKITAKA WAACHWE…. MZUNGU WA YANGA PRINCESS MAMBO NI ‘BULL BULL’….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply