Simba SC

KAGERA SUGAR: SIMBA WAMETUONYESHA DHARAU TATU KWA MHILU

admin August 21, 2021 11:43 am


UONGOZI wa Kagera Sugar umeweka wazi kuwa mabosi wa Simba walionyesha dharau kubwa kwenye usajili ya mchezaji wao Yusuph Mhilu ambaye amesaini dili la miaka mitatu ndani ya Simba.

Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamis Manzanzala amesema kuwa mabosi hao wameonyesha darau tatu ikiwa ile dharau ya kwanza wamefanya mazungumzo na mchezaji bila idhini yao, pili wamemsainisha mchezaji mkataba bila idhini yao,tatu wamemtangaza Yusufu Mhilu bila idhini yetu huku ni kutudharau.


“Mhilu alikuwa anamkataba na sisi wa mwaka mmoja kubaki na katika mkataba wake kulikuwa na kipengele cha kusajili na kumtumia mdogo wake Dickson Mhilu kitu ambacho tulikifanya, Simba hawawezi kumtumia Mhilu mpaka sisi tuamue.

“Wao wameshamsainisha Mhilu sasa wanakujaje kutaka kufanya mazungumzo, tumeingia gharama kubwa kumtengeneza Yusuph Mhilu gharama yake ni kubwa.”


Chanzo:RFA



VIDEO: HASSAN MWAKINYO ANAZUNGUMZA MUDA HUU PAMOJA NA CORONA, FAMILIA WAITAJA MECHI YA SIMBA VS YANGA CHANZO CHA KIFO MWL KASHASHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply