NYOTA watatu wa Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England kwa sasa wanapatiwa matibabu ili waweze kurejea kwenye ubora baada ya kukutwa na virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo hivi karibuni.
Ni nahodha wao Pierre Emerick Aubameyang, Alexandre Lacazette na Alex Runarsson ambao wameripotiwa na uongozi wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta kwamba walikuwa na Corona.
Kesho Jumapili Arsenal ina kibarua cha maana kusaka pointi tatu mbele ya Chelsea na utakuwa ni mchezo wao wa pili kwenye Ligi Kuu England wakiwa wanakumbuka kwamba walinyooshwa mabao 2-0 dhidi ya Brentford kwenye mchezo wa kwanza.
Arsenal wametoa taarifa kwamba wachezaji hao walikuwa na Corona hata kabla ya mchezo wa wikiendi iliyopita lakini Aubameyang atakuwepo kwenye mchezo huo baada ya kupimwa na kukutwa hana virusi huku wengine wawili Lacazette na Runarsson bado hawajawa fiti.