Simba SC

WAKATI YA MHILU HAYAJAPOA…KOCHA GWAMBINA AIBUKA NA HILI KUHUSU STAA MPYA WA SIMBA

admin August 23, 2021 2:00 am


JIMMYSON Mwanuke ametua Simba, huku baadhi ya mashabiki wakijiuliza atauweza mtiti wa pale Msimbazi, lakini kocha wake wa zamani aliyemnoa Gwambina, Mohammed Badru amesema Wekundu hao wamelamba dume kwa winga huyo na huenda akawasahaulisha Luis Miquissone.

Badru alisema Mwanuke ni winga aliyekamilika na alikuwa kwenye mipango yake ndani ya Mtibwa Sugar anayoinoa kwa sasa, ila Simba wamemuwahi na kusema hawatajutia kumsajili kwani soka analijua na hata umri wake unambeba mbele ya wenzake.

“Namjua ni mchezaji mzuri kwani nimemfundisha Gwambina, nilipenda kumtumia kama mchezaji wa kubadili matokeo, kama Simba itakuwa na uvumilivu na kumpa nafasi kuizoea timu atawasaidia kwani aina ya uchezaji wake ni kama Mrisho Ngassa aliye kwenye ubora wake,” alisema Badru.

Mwanuke ni mchezaji wa pili aliyeyeyuka kwenye mipango ya Badru, mwingine akiwa ni Said Juma Makapu aliyeachwa Yanga na kutua Polisi Tanzania.

TANO BORA YA UTUPIAJI, SIMBA WATAWALA BAADA YA KUONA WACHEZAJI WAPYA..NABI AGUNA KISHA AOMBA MUDA YANGA..AMTAJA GSM

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply