Simba SC

KUELEKEA SIMBA DAY MSIMU HUU..UONGOZI SIMBA WAJA NA HILI JIPYA

admin August 24, 2021 2:00 am

 


KIKOSI Bora, hiyo ni kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ akiwataka mashabiki wao kukaa mkao wa kula kuiona timu yao.

Kikosi cha Simba kipo nchini Morocco kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa sambamba na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza akiwa Morocco Try Again amesema, kambi yao iko salama na maandalizi makubwa ambayo wameyafanya.

Amesema kocha wao Didier Gomes alitaka kupata utulivu wa hali ya juu akiwa na wachezaji wake ili kuijenga timu vilivyo.

”Kocha amepata utulivu wa hali ya juu na wachezaji wake kwa ajili ya kuandaa kikosi bora ambacho kitafanya vizuri Sana, “

Amesema Simba msimu ujao itakuwa tishio zaidi ya msimu uliopita kutokana na namna ambavyo wamefanya maandalizi ya kutosha na yenye utulivu mkubwa.

Aidha Try Again amewataka wanasimba kukaa mkao wa kula kuishuhidia timu yao katika tamasha la Simba Dar linalotarajiwa kurindima mwezi ujao katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Awali Simba walitarajia kufanya tamasha hilo Agosti 28 mwaka huu lakini imeshindikana kutokana na ratiba kubana ikiwemo timu za Taifa pia.

Hata hivyo Simba mpaka sasa hawajatangaza tarehe rasmi ya kufanyika kwa tamasha hilo huku habari za chini chini zinasema huenda likafanyika Septemba 4 au 11

BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA..TSHISHIMBI AUTAKA URAIA WA TZ AICHEZEE TAIFA STRAS MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply