news

KIPA LIGI KUU BARA MAMBO YAKIWA MAGUMU KUGEUKIA UDAKTARI

admin August 25, 2021 2:44 pm


 MUSSA Mbissa kipa namba moja ambaye aliokota mabao mengi nyavuni kwa msimu wa 2020/21 amesema kuwa mambo yakiwa magumu kwenye soka atarejea kwenye fani yake ya udaktari.

Nyota huyo ambaye ni mali ya Mwadui FC anakumbuka aliweza kuokota mabao matanomatano alipokutana na Simba na Yanga huku akiwa ni kipa wa kwanza kuokota mabao matatu kutoka kwa mchezaji mmoja, ‘hat trick’.

Ilikuwa ni mbele ya JKT Tanzania wakati ubao wa Mwadui Complex uliposoma, Mwadui FC 1-6 JKT Tanzania na aliyemtungua mabao matatu alikuwa ni Adam Adam.

Kipa huyo ambaye alikubali kuokota jumla ya mabao 57 kwenye nyavu zake amesema kuwa hawezi kuusahau msimu wa 2020/21 kwa kuwa ni kipa ambaye amefungwa mabao mengi.

“Ikitokea masuala ya mpira yamegoma basi ninaweza kurejea kwenye fani yangu ambayo nilisomea ya udaktari.

“Kama kwenye mpira nitafeli basi nitarudi kwenye taaluma yangu ya udaktari,” amesema.

NABI: BADO TIMU HAIJAPATA MUUNGANIKO KWA SASA VIDEO: JUMA KASEJA, NAHITAJI HESHIMA TU,ATAJA UCHAWI WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply