Yanga SC

NABI: BADO TIMU HAIJAPATA MUUNGANIKO KWA SASA

admin August 25, 2021 12:43 pm


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amebainisha kwamba bado timu yake haijawa na muunganiko bora licha ya kwamba ilikuwa imeweka kambi nchini Morocco.

Jana, Agosti 24 kikosi cha Yanga kilirejea Dar baada ya kuvunja kambi yao iliyokuwa nchini Morocco kwa kile walichoeleza kuwa ni maslahi mapana ya Yanga.

Maandalizi yao kuelekea msimu wa 2021/22 sasa yatakuwa ni Kigamboni katika kijiji cha Avic Town.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Nabi amesema;-“Muunganiko wa timu bado, tunahitaji muda kama mwezi au miezi mitatu kwa sababu timu haijengwi kwa muda mfupi.

“Wachezaji wote tuliowasajili ni wazuri kwa sababu tulikuwa tunawafuatilia, tukipata muda zaidi tutakuwa bora zaidi,” amesema Nabi.


GOMES AFURAHISHWA NA UWEZO WA WACHEZAJI WAKE KIPA LIGI KUU BARA MAMBO YAKIWA MAGUMU KUGEUKIA UDAKTARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply