Simba SC

GOMES AFURAHISHWA NA UWEZO WA WACHEZAJI WAKE

admin August 25, 2021 12:43 pm


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi ya msimu ujao yanakwenda vizuri huku akifurahishwa na uwezo wa wachezaji ambao wanauonyesha.

Mchezo mmoja wa kirafiki Gomes aliwaongoza vijana yake ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya FAR Rabat ya Morocco ambapo ulikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Baadhi ya wachezaji wa Simba wameondoka kambini na kujiunga na timu za taifa huku baadhi wakiendelea kuwa na kambi nchini Morocco na miongoni mwa nyota hao ni Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Chris Mugalu, Ally Salim.

Raia huyo wa Ufaransa amesema:”Kila kitu kina kwenda sawa na maandalizi yapo vizuri jambo ambalo linaleta matumaini kwa ajili ya msimu mpya.

“Kila mchezaji anatimiza majukumu yake na hilo ni jambo la msingi hivyo imani yetu ni kuona kwamba tunakuwa na wakati mzuri kwa wakati ujao,” .

HUU HAPA UZI MPYA WA YANGA, MANARA AUTAJA KUWA BORA NABI: BADO TIMU HAIJAPATA MUUNGANIKO KWA SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply