news

AL AHLY WAMTAMBULISHA KIBABE MIQUISSONE..KUMBE SIMBA WAMELIPWA MPUNGA HUU..

admin August 26, 2021 6:30 pm


Hatimaye Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly wamemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone, akitokea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Miquissone amejiunga na miamba hiyo ya soka Barani Afrika kwa ada ya uhamisho inayotajwa kufikia Dola za Kimarekani laki tisa ($900,000) ambazo ni zaidi bilioni 2 kwa pesa za Tanzania.

Ada hiyo ya uhamisho inamfanya Miquissone kuweka Rekodi ya kuwa mchezaji alieuzwa kwa pesa nyingi zaidi kwenye historia ya Soka la Bongo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, alionesha kiwango cha hali juu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika akiwa na Simba SC, huku akifunga bao la ushindi dhidi ya Al Ahly timu hizo zilipokutana jijini Dar es salaam.

BREAKING: RASMI LUIS MIQUISSONE ATAMBULISHWA AL AHLY YA MISRI SAMUEL ETO’O NEMBO YA AFRIKA ILIYOSUMBUA ULIMWENGU WA MICHEZO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply