UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hakuna kinachoshindikana kuhusu ishu ya nyota wa Simba Luis Miquissone anayetajwa kutua hapo kwa mkopo akitokea Klabu ya Al Ahly ya Misri.
Kumekuwa na tetesi kuwa Luis ambaye tayari amewaaga Simba kuwa hatakuwa nao msimu ujao wa 2021/22 huenda akaibuka ndani ya Yanga kwa mkopo kwa kuwa anatajwa kuuzwa Al Ahly ya Misri ambao wao wemeamua kumtoa kwa mkopo.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kuwa ni suala la mashabiki wa Yanga kusubiri nini kitatokea kwa kuwa muda bado upo kwa sasa na kila kitu kitajulikana siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi, Agosti 29.
“Siku hiyo tutakuwa na sapraizi nyingi sana kwa mashabiki, kuhusu suala la kumchukua Luis kwa mkopo kutoka Al Ahly hakuna kitu kunachoshindikana, hivyo watu waendelee kusubiri wanachotakiwa ni kuhudhuria Tamasha la Wiki ya Mwananchi, “.
Bado haijawa rasmi kwamba Luis Miquissone anaweza kujiunga na Al Ahly kwa kuwa uongozi wa Simba ulibainisha kuwa timu iliyomchukua iliomba asitambulishwe kwanza ila uhakika ni kwamba Luis anasepa Simba.
Chanzo: Spoti Xtra