Simba SC

BAADA YA WIKI MBILI MOROCCO…SIMBA KURUDI BONGO KISHA..WATASEPA TENA MAJUU

admin August 27, 2021 10:01 pm


Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kitarejea Dar es salaam mwishoni mwa juma hili kikitokea Morocco.

Kaimu Afisa Habari wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amethibitisha taarifa za mpango wa kurudi nchini kwa kikosi chao ambacho kimeweka kambi kwa majuma mawili mjini Rabat, Morocco.

Kamwaga amesema baada ya kuwasili nchini wachezaji watapata mapumziko ya siku chache, kisha watarejea kambini katika moja ya nchi za bara la Afrika.

Hata hivyo Kamwaga hakutaka kuweka wazi nchi na mahala ambapo kikosi chao kitakwenda kuweka kambi ya kuendelea na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

WAJUE WALIOPIGWA ‘PANGA’ SIMBA, MANARA ANAWAKERA ,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI KISA WACHEZAJI WAPYA…GOMES AVUNJA UKIMYA MSIMBAZI…AMTAJA CHAMA NA MIQUISSONE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply