Simba SC

RASMI..MAGORI AVUNJA UKIMYA VITA YA BARBRA NA MANARA..AFUNGUKA KUHUSU UTAJIRI WA MO DEWJI

admin August 28, 2021 5:00 pm


Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’, amemjibu Haji Manara kwa kueleza uhalisia wa tajiri huyo.

Crescentius Magori, Mshauri wa Mohamed Dewji ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, amesema kinachoendelea kwa mtu mmoja kuzungukaa na kuzungumza upuuzi, hakitaiyumbisha klabu yao.

Magori amesema: “Kuna watu wanazunguuka kwenye Media na kusema Mohamed Dewji ni tajiri wa mitandaoni, eti kisa matajiri wengine hawaonekani mitandaoni, “

“Napenda kuwajibu kwamba hiyo ndiyo life style ya MO na mimi kama mshauri wake namshauri asibadilishe Style ya maisha yake kwa kuishi wanavyotaka watu wengine.”

“Tunajua yote yanaendelea huko ni kutaka kumdhoofisha Mohamed Dewji ‘Mo’ ili waidhoofishe Simba SC. Yaani ni propaganda za kizamani.”

“Niwahakikishie wamegonga mwamba Mohamed anasema hatotetereka wala hatoyumbishwa na maneno ya mtu yeyote, yeye anaijenga Simba SC ifike ambako inastahili pia amehaidi ni lazima Simba SC ya msimu ujao ipige hatua zaidi ya msimu uliopita. Na kuhusu Makombe tutachukua na Tutachukua tena.”

Magori ambaye alikua sehemu ya viingozi waliokuwa kambini nchini Morocco, kwa sasa yupo safarini kurejea jijini Dar es salaam.

MAKAMBO, DJUMA NA MAYELE WAVUNJA REKODI YANGA…MZEE MPILI AKIIBUKA KWA STAILI MPYA RASMI…KISINDA ATAMBULISHWA KIBABE HUKO MOROCCO..MIAKA YAKE HALISI YATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply