Azam FC

AZAM FC KAMBI YAZIDI KUIMARIKA ZAMBIA, WAITUNGUA KABWE WARRIORS

admin August 30, 2021 7:43 am


 ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa maandalizi ya msimu wa 2021/22 yanakwenda vizuri kutokana na kuwa na mpango kazi maalumu ambao unafanyika.

Kwa sasa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kimeweka kambi nchini Zambia ikiwa ni kwa ajili ya kuwafanya wawe bora zaidi ya msimu uliopita.

Thabit ambaye wengi hupenda kumuita Zakazaki amesema kuwa wanatambua kwamba msimu ujao utakuwa na ushindani jambo ambalo linawafanya wapange kufanya vizuri.

“Tupo vizuri na kila kitu kinakwenda sawa, kikubwa ni kuona kwamba tunakuwa imara, kambi na kila kitu huku Ndola kinakwenda sawa,” amesema.

Jana, Azam FC ilicheza mchezo wa pili wa kirafiki ilikuwa dhidi ya Kabwe Warriors na ilishinda kwa bao 1-0.

RUVU SHOOTING YAIPIGIA HESABU TANO BORA HUU HAPA UKWELI KUHUSU ”MAHUSIANO YA KI…ZI..” KATI YA MANARA NA MWAMNYETO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply