ALIYEKUWA kipa wa Yanga, Faruk Shikhalo amejiunga na klabu ya KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo.
Mtu wa karibu na mchezaji huyo alithibitishia kwamba Shikhalo amesaini mkataba huo na anatarajia kwenda kujiunga na wenzake kambini.
โShikhalo ameshasaini na KMC, timu ipo Morogoro yeye anakamilisha baadhi ya vitu ili aende akajiunge na wenzake,โ kilisema chanzo hicho.
Shikhalo anaenda kukutana na kipa mkongwe, Juma Kaseja ambaye amejihakikishia nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha KMC.
Kipa huyo aliachana na Yanga baada ya kutoongezewa mkataba yeye na mwenzake Metacha Mnata huku nafasi zao zikichukuliwa na Diarra Djigui na Erick Johola.