Uncategorized

NYOTA SPURS AWAFUATA MASHABIKI NA KUZOZANA NAO

admin March 5, 2020 5:35 am


NYOTA wa kikosi cha Tottenham Spurs, Eric Dier, usiku wa kumkia leo aliwafuata mashabiki na kuzozana nao baada ya timu yake kutolewa kwenye mchezo wa Kombe la FA, England na Norwich kwa penalti 3-2.

Licha ya Spurs kuanza kushinda dakika ya 13 kupitia kwa Jan Vertonghen bao hilo lilisawazishwa na Josip Drmic dakika ya 78 liliwapeleka kwenye hatua ya changamoto ya penalti ambapo Spurs ilifunga 2-3 za Norwich City.

Nyota huyo alifanya hivyo baada ya kuhisi kwamba Kaka yake alikuwa anabezwa na mashabiki kwa kitendo cha timu hiyo kushindwa kutinga robo fainali ya Kombe la FA England.

Kwa kitendo hicho nyota huyo adhabu inamuhusu. Kocha Mkuu wa Spurs, Jose Mourinho amesema kuwa familia ya Eric ilikuwa ndani ya uwanja na Kaka yake alifanyiwa kitu kisichopendaza lakini Eric naye amefanya jambo ambalo mchezaji hapaswi kufanya ila imetokea.

AZAM FC YAKWAMA KUFUTA UTEJA KWA SIMBA, SASA NGUVU ZA SIMBA KWA YANGA SPIDI YA NAMUNGO INASTAHILI PONGEZI LAKINI KAMA KUNA MCHANGANYO WA SIASA ANGUKO LINAKUJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply