Yanga SC

Yanga Yaendelea Kusafisha Kikosi, Damaro Kwenye Mlango Wa Kutokea

Vardo July 4, 2026 2:28 pm

KIUNGO wa Yanga, Mohamed Damaro, anatarajiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaotarajiwa kuachwa kuelekea msimu wa 2026/27.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa uongozi wa Yanga umeanza mchakato wa kufanya maboresho makubwa ya kikosi, ukilenga kuongeza ushindani na ubora, hususan katika eneo la kiungo, kupitia usajili wa nyota wapya.

Damaro, ambaye alisajiliwa kwa matarajio ya kuimarisha safu ya kiungo, inaelezwa kuwa hayupo tena kwenye mipango ya benchi la ufundi baada ya tathmini ya kikosi kuelekea msimu mpya kukamilika.

“Uamuzi huo ni sehemu ya mkakati mpana wa Yanga wa kufanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi muhimu, ikiwa ni maandalizi ya kushindana kwa nguvu zaidi kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa,” amesema mtoa habari huyo.

Amesema kuondoka kwa , Damaro atahitimisha safari yake ya kuitumikia Yanga na ataanza kutafuta changamoto mpya katika maisha yake ya soka.

Hadi sasa Yanga haijatoa tamko rasmi kuhusu hatma ya kiungo huyo, hivyo taarifa za kuondoka kwake bado zinasubiri uthibitisho kutoka kwa uongozi wa klabu.

Sifu Amon Kuamua Hatma Ya Kombe La CRDB Gombani Yanga Yazindua Vita Ya Taji La Sita Mfululizo, Hersi Afichua