Simba SC

Sifu Amon Kuamua Hatma Ya Kombe La CRDB Gombani

Vardo July 4, 2026 2:13 pm

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Sifu Amon wa Mbeya kuwa mwamuzi wa kati wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank kati ya Simba SC na Azam FC itakayochezwa leo, Julai 4, 2026, kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, kuanzia saa 11:00 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Sifu Amon ndiye atakayeongoza mchezo huo wa dakika 90, akisaidiwa na waamuzi wasaidizi Hamdani Said wa Mtwara na Zawadi Yusuph wa Dar es Salaam. Mwamuzi mwenye uzoefu Ahmed Arajiga kutoka Manyara amewekwa kuwa mwamuzi wa akiba.

Katika upande wa usimamizi wa mchezo, Athumani Kambi wa Mtwara atakuwa Kamishna wa mechi, huku Kassim Haji wa Tanga akihudumu kama Kamishna Mkuu. Mkaguzi wa waamuzi ni Soud Abdi kutoka Arusha.

Kwa upande wa teknolojia ya Video Assistant Referee (VAR), Hashim Abdallah wa Dodoma ndiye atakayesimamia VAR akisaidiwa na Karim Boimanda wa Dar es Salaam, wakati Cliford Mario Ndimbo akiwa msimamizi wa uendeshaji wa mfumo huo.

Fainali hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Simba na Azam FC zikisaka taji la mwisho la msimu wa 2025/26, jambo linaloweka presha kubwa kwa waamuzi kuhakikisha mchezo unasimamiwa kwa haki, weledi na kuzingatia Sheria za Mpira wa Miguu.

Maumivu Ya Dakika Ya 86 Timu Tatu Afrika Yanga Yaendelea Kusafisha Kikosi, Damaro Kwenye Mlango Wa Kutokea