Paredi La Ubingwa Yanga Laibua Mambo
WAKATI Yanga ikisherehekea ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kufanya paredi leo Jumamosi ya Julai 4, 2026, mashabiki kadhaa wa timu hiyo wameonekana Kutoridhishwa na utaratibu uliotumika wa maandalizi hayo.
Mashabiki hao wamekuwa wakikosoa utaratibu uliotumika kuweka eneo la Karume ambalo wanaamini ni dogo na halina hadhi kwa kuanzisha paredi hilo kama ilivyokuwa utaratibu wa misimu yote inayofanya kikosi hicho kilipotwaa ubingwa.
Kwa misimu ya hivi karibuni, shughuli hizo zimekuwa zikianzia Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, japo safari hii mambo yamekuwa ni tofauti na inaanzia Karume, ikipita Msimbazi iliko makao makuu ya Simba na kuhitimisha mitaa ya Twiga na Jangwani yalipo makao makuu ya kikosi hicho.
Minong’ono hiyo inajiri baada ya uongozi wa Yanga kutangaza paredi hilo litaanza saa 4:00 asubuhi, ingawa hadi sasa saa 11:40, bado halijaanza.