Simba SC

PETER BANDA AITWA TIMU YA TAIFA YA MALAWI

admin August 30, 2021 12:43 pm


 BAADA ya kumaliza maandalizi ya kwanza kuelekea msimu mpya wa 2021/22 na kurejea Tanzania, kiungo  wa Simba Peter Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes iliweka kambi kwa muda nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Banda ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Malawi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022. 

Pia wapo nyota wengine wa Simba ambao wapo kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania ambao ni pamoja na Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein pamoja na John Bocco.


BAADA YA KUMALIZA MSIBA..BENO KAKOLANYA AWALILIA MASHABIKI WA SIMBA..AFUNGUKA HAYA VIDEO:JULIO AWAPONGEZA YANGA KWA SHUGHULI YA WIKI YA MWANANCHI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply